Exercise 6

Take a song or poem in any language of your country and translate it into English. Try to translate the meaning accurately, even if the literary form in English is different. The Kiswahili poems given below are suitable for those who know Kiswahili.

As in EXERCISE 1, underline every place in your translation where you have used an idiomatic expression or grammatical construction that is different from that of the Source Language. Discuss these with an advisor or colleague.

Underline every place in the original where there is a poetic or literary device that you have been unable to put into English. How does this change the effect or impact of the song or poem?

Could your translation be sung to the same melody as it can be sung in the Source Language? How might it be adjusted so that it can be sung?

Excerpt from KUKU NA MWEWE
The Chicken and the Hawk, by K W Wamitila, Muwa Publishers Limited, 2006.

Paukwa!
Paukwa!

Nyakati zilizopita, hizo zama za zamani,
Njaa iliwakeketa, wanyama wote mwituni,
Nyani, sungura na bata, wakengia taabani,
Wakaulizana kwani, sasa tutafanya nini?

Wakazipiga akili, wanyama wote porini,
Kupima lile na hili, wafanye shauri gani?
Njaa imewakabili, hawana mlo nyumbani,
Wakaulizana kwani, sasa tutafanya nini?

Sungura kajitokeza, kaingia ukumbini,
Kasema, “inashangaza, sisi akina fulani,
Njaa inatuchakaza, mwewe kiruka angani,”
Wakaulizana, “kwani, sasa tutafanya nini?”

“Mimi vile ninaona, mwewe akiwa angani,
Kote anawezaona, kote kote aridhini,
Chakula anakiona, akiwapo mawinguni,”
Wakaulizana kwani, sasa tutafanya nini?

Wakatoa na mawazo, wote pale ukumbini,
“Ni nani siri anazo, za kutupaza angani?
Na tuone siri hizo, tutie kitu tumboni,”
Wakaulizana kwani, sasa tutafanya nini?


Excerpts from UTENDI WA AYUBU
Ballad of Job, a classical Swahili ballad

Mtume wetu Ayubu
apeweo na Wahabu
mali mangi ya ayabu
      yakaenea dunia

Kwanda na tutaye mbuzi
yali alifu mazizi
alopowa na Azizi
      mangi mali yasosia

Na watumwa wa kukifu
kulla zizi maarufu
wali watunga alifu
      waliokimtungia

Na ng’ombe na ngamiaze
na farasi na pundaze
hesabuye niweleze
      ni kama nimezotaya

Na anwai na mali
kulla kitu mbalimbali
kuzitaya ni muhali
      siwezi kuwatayia

Na wanawe tuwaseme
ni sabaa wanaume
kana simba wenye tume
      wote marika mamoya

Na watatu wanawake
wenye nuru taambake
jumla zijana zake
      ashara metimilia

Umuwshiye Wadudi
ibada akashtadi
kwa mali na auladi
      yasimpe kushangaa

Akendo mno ibada
kwa Molawe Sarimada
pakaitoka husuda
      ya kuya kuhusudia

Kisha cha tumwa Ayubu
nimekoma kukutubu
kwa auni ya Wahabu
      Rabbi menisahilia

Ameifanya sahali
illahi Rabbi Jalali
kiarabu kubadili
      lugha ya kiswahilia

Tumeyanoa zuoni
na katika Quruani
na nyinyi angaliani
      sikusaza neno moya


Hiki Si Kile
by Ahmad Nassir bin Juma Bhalo

Natamba mtambi tambo           na watambi hatambile
hajifungata masombo           kwa hayano na hayale
nakuwaonya vigambo           ukumbi wa watu tele
hiki na hiki si kile           hikino ni kiki hiki.

Yaweni yasiyokuwa           yaweni yawe yawele
huko ni kujiatuwa           pelelezato uole
mambo ni majaaliwa           kiumbe sisahawile
hiki na hiki si kile           hikino ni kiki hiki.

Siwi bangu habananga           mwendo wangu ni u’ule
bongo langu limejenga           akili kitwani tele
sipigani na mjinga           nyuma akwitaye mbele
hiki na hiki si kile           hikino ni kiki hiki.

Dunia ichigaluka           penye mafupi na male
wakumbwa hupapatika           leo hivi kesho vile
ni wapi pa kuwaweka           dhiki zisiwadhikile
hiki na hiki si kile           hikino ni kiki hiki.

Tammati baiti tano           shairi nalikomele
sipendi kusema nao           ningaweza kwenda mbele
mwisho wangu ni hapano           ajuaye n’atambule
hiki na hiki si kile           hikino ni kiki hiki.

REMEMBER:
When checking a translation, ask:
Is it accurate? Is the meaning as nearly as possible the same meaning that the original author intended?
Is it clear? Will people understand the message?
Is it natural? Is this the way that people speak?


Adapted from Bible Translation: An Introductory Course in Translation Principles by Katharine Barnwell, 2017, page 32.